Walimu waliopandishwa 126,346
Kufuatia agizo la Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilolitoa tarehe 1 Mei, 2021 katika sherehe za siku ya wafanyakazi, kuwa watumishi wa umma wenye sifa za kupanda vyeo wapandishwe, TSC ilipandisha walimu 126,346 wa shule za Msingi na Sekondari. Idadi hii ni imejumuisha Ikama ya miaka mitatu mfululizo yaani 2018/2019, 2019/2020 na 2020/2021. Kutokana na mwongozo uliotolewa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (MUUUB) juu ya namna ya kuendesha zoezi hilo, TSC ilipandisha walimu wote waliokuwa na sifa za kupanda.