Majukumu ya Tume

Majukumu ya Tume ya Utumishi wa Walimu yameainishwa kwenye Kifungu Na. 5(i) – (xii) cha Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu Na. 25 ya Mwaka 2015 ambayo ni:-

 1. Kuendeleza na kusimamia Utumishi wa Walimu;

 2. Kumshauri Waziri juu ya kusimamia na kuendeleza Utumishi wa Walimu;

 3. Kuajiri, kupandisha vyeo na kuchukua hatua za kinidhamu kwa walimu;

 4. Kuhakikisha uwiano sawa katika usambazaji wa Walimu ndani ya Serikali za Mitaa na Shule;

 5. Kushughulikia masuala ya rufaa zinazotokana na maamuzi ya Mamlaka ya Nidhamu;

 6. Kutunza daftari la kumbukumbu za walimu wote waliopo kwenye Utumishi wa Umma;

 7. Kusimamia programu za mafunzo ya walimu kazini;

 8. Kufanya utafiti na tathmini kuhusu masuala yanayohusu Utumishi wa walimu na kumshauri Waziri inavyostahiki;

 9. Kutathmini hali ya Walimu na kushauri Wizara yenye dhamana ya masuala ya walimu juu ya mafunzo, idadi na uhitaji wa walimu nchini;

 10. Kuandaa Kanuni za Maadili ya Utendaji kazi ya mwalimu;

 11. Kuendeleza mfumo wa mawasiliano na Ofisi za Tume katika ngazi ya Wilaya juu ya mambo yote au jambo lolote kuhusiana na maendeleo ya Utumishi wa walimu na kuhakikisha kwamba Mwajiri na Ofisi ya Tume ngazi ya Wilaya wanatekeleza kazi zao kwa mujibu wa Sheria; na

 12. Kufanya jambo lolote ambalo kwa maoni ya Waziri linafaa au kutegemewa katika utekelezaji bora wa kazi za Tume.