Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa

Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Kuna aina nne za Maktaba zinazosimamiwa na TLSB ambazo ni Maktaba Kuu ya Taifa, Maktaba za Mikoa, Maktaba za Wilaya na Maktaba za Tarafa.
TLSB kwa sasa ipo katika mpango wa kuuboresha mfumo wake wa  huduma za Maktaba kwa kuuendeleza, kuusimika na kuusimamia mfumo wa Maktaba Mtandao wa Taifa  (Integrated National  Digital Library System)  kwa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) .
Ndani ya kipindi kilichopo,TLSB inatarajia kusimamia mradi wa kukarabati jengo la makao makuu yake iliyopo Dar-es-Salaam pamoja na kujenga maktaba mpya mbili zitakazokuwepo wilayani Chato na Mkoani Arusha.
Msingi Mkuu wa TLSB ni Ubora; Uwajibikaji na Uwazi; Viwango vya Maadili na Uadilifu; Ubunifu, Usawa na Ubia na Ushirikiano. 
Mwaka 1975, Sheria hiyo ilirekebishwa ambapo Sheria mpya ya Bunge Namba 6 ya   mwaka 1975 iliundwa na kupelekea jina la Taasisi kubadilika kutoka Bodi ya Huduma za Maktaba Tanganyika na kuwa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania .
Lengo kuu la kuundwa kwa TLSB lilikuwa kutoa fursa kwa wananchi wote bila ubaguzi wa     aina yoyote, kutumia Maktaba za Umma ili kujipatia elimu, maarifa na taarifa mbalimbali  zitakazowasaidia katika kujikwamua kutoka katika umasikini na ujinga na pia kupata     ...
Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB) ni Taasisi ya Umma iliyopo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Taasisi hii ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Namba 39 ya mwaka 1963 ikijulikana kama Bodi ya Huduma za Maktaba Tanganyika.
Makao Makuu ya Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB) yapo makutano ya Barabara ya Bibi Titi, Mohamed na Barabara ya Azikiwe, Posta - Dar es salaam