Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
UKARABATI WA TLSB MAKAO MAKUU DAR ES SALAAM
08 Nov, 2022
service image
Meneja Mradi wa Ukarabati TLSB Mhandisi Mayenga Magembe wa Halmashauri ya Jiji Ilala, amekabidhi maeneo yatakayofanyiwa ukarabati Maktaba Kuu ya Taifa Dar es Salaam kwa Local Fundi, ili kuanza zoezi hilo la ukarabati hivi karibuni. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za TLSB Makao Makuu Dar es Salaam tarehe 14 Septemba 2022. Katika zoezi hilo Mhandisi Magembe aliambatana na Meneja Mradi Msaidizi Mhandisi Rosemary Tendeka. Kwa upande wa TLSB, makabidhiano hayo yamesimamiwa na Afisa Miliki Bw. Gerald Elia. Aidha, Wafanyakazi kutoka Idara na Vitengo mbalimbali TLSB wameshuhudia makabidhiano hayo.