Majukumu
Majukumu ya Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania yanatekeleza matakwa ya sheria ya Bunge Namba 6 ya mwaka 1975. Majukumu hayo ni:
- Kuanzisha, kuendesha, kuongoza, kuboresha, kutunza na kuendeleza Maktaba za umma kote nchini kuanzia ngazi za mikoa, wilaya hadi tarafa.
- Kuupatia umma wa Watanzania taarifa mbalimbali zilizokusanywa kutoka katika ulimwengu mpana wa maarifa kwa ajili ya elimu, utafiti na maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.
- Kukusanya na kuhifadhi machapisho ya kitaifa.
- Kutoa mafunzo na kuendesha mitihani ya taaluma ya Ukutubi kwa wafanyakazi wa Bodi, Maktaba za shule, vyuo na taasisi mbalimbali nchini.
- Kuanzisha, kukuza, kusimamia, kuratibu na kuendeleza huduma za maarifa na utafiti (documentation services) nchini.
- Kutoa ushauri na uelekezi kwa idara za serikali, taasisi na mashirika mengine kuhusu kuanzisha, kuendeleza na kuboresha huduma za Maktaba katika maeneo yao.
- Kuendesha mfumo wa ushirikiano kati ya Maktaba za Umma na Taasisi nyingine zinazotunza nyaraka ili kuwawezesha wananchi kupata taarifa kwa gharama nafuu.