Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa

HOTUBA YA WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA PROF. ADOLF FAUSTINE MKENDA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2022/23

07 Nov, 2022 Pakua
Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lakoTukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii iliyochambua makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia FUNGU 46 na FUNGU 18 la Tume ya Taifa ya UNESCO, naomba kutoa hoja kwamba sasa Bunge lako Tukufu, likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia FUNGU 46 na FUNGU 18 kwa mwaka wa fedha 2021/22. Aidha, naliomba Bunge lako Tukufu likubali kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2022/23.