Divisheni ya ufundi inajishughulisha na uandaaji, uagizaji, utayarishaji na usambazaji wa machapisho katika Maktaba za Mikoa, Wilaya na Tarafa. Pia inatoa huduma kwa Vyuo, Taasisi za Serikali na zisizo za Kiserikali, Shule (za Sekondari na Msingi) na NGO’S ambao wamejiunga uanachama wa Maktaba.
Pia Kutoa ushauri wa namna ya kuanzisha Maktaba na jinsi ya kuziendeleza, na kusimamia usambazaji wa machapisho kwenda kwenye maktaba za Mikoa, Wilaya na Tarafa.