Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
KONGAMANO LA PILI LA KITAIFA LA HUDUMA ZA MAKTABA, MAONESHO YA VITABU NA USOMAJI 2022
07 Nov, 2022
service image
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB) anawaalika wananchi wote katika Kongamano la Pili la Huduma za Maktaba za Taifa, Maonesho ya Vitabu, na Tamasha la Usomaji, litakalofanyika katika ukumbi wa Tanga Beach Resort and Spa, kuanzia Novemba 23 hadi Novemba 24, 2022, Tanga. “Nitumie fursa hii kuwakaribisha wananchi wote kuhudhuria Kongamano hili ili kupata uelewa mpana wa shughuli mbalimbali nzuri zinazofanywa na TLSB,” alisema Dk.Ruzegea. Aidha, katika Kongamano hili, mada mbalimbali; itatolewa sambamba na Maonesho ya Vitabu na Tamasha la Kusoma, ambapo wananchi watasoma vitabu vya kiada na ziada kutoka kwa washiriki wengine. Kongamano hilo lina kauli mbiu ''Mafunzo ya Maktaba, Huduma ya Habari na Nyaraka katika Muktadha wa Mabadiliko ya Elimu Tanzania'' lilizinduliwa rasmi mwaka 2021 jijini  Dodoma na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa Maktaba.