Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Uboreshaji wa Daftari

Kwa mujibu wa Kifungu cha 15(5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kifungu cha 21(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Tume inatakiwa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mara mbili kati ya Uchaguzi Mkuu uliomalizika na unaofuata. Wanaohusika katika zoezi hili ni wananchi ambao: -

  1. Wametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea ambao hawakuandikishwa hapo awali;
  2. Watakaotimiza miaka 18 wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020;
  3. Waliojiandikisha awali na wamehama Kata au Jimbo moja kwenda jingine;
  4. Waliokosa sifa mfano wale waliofariki kuondolewa katika Daftari;
  5. Wenye taarifa zilizokosewa wakati wa uandikishaji; na
  6. Waliopoteza au kadi zao kuharibika.

Watendaji wa Uandikishaji/ Uboreshaji

Tume ya Taifa ya Uchaguzi hutumia watendaji mbalimbali wakati wa Uandikishaji na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Watendaji hawa ni pamoja na:-

  1. Waratibu wa Uchaguzi wa Mkoa;
  2. Maafisa Waandikishaji;
  3. Maafisa Waandikishaji Wasaidizi;
  4. Waandishi Wasaidizi; na (v) ‘’BVR Kit Operators’’.

Mawakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura

Kwa mujibu wa Kifungu cha 15A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, na Kifungu cha 17A cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 Chama cha Siasa chenye usajili wa kudumu kinaweza kumteua mtu mmoja katika kila kituo cha uandikishaji kuwa Wakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura.

Wajibu/Majukumu ya Mawakala wa Uandikishaji

  1. Kufuatilia zoezi la uboreshaji na kutazama kama linazingatia Sheria, Kanuni na Maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
  2. Kushirikiana na Waandishi Wasaidizi kutambua wakazi wa eneo hilo na kutoa taarifa juu ya watu wasio na sifa.

Pamoja na majukumu tajwa, Mawakala wa Uboreshaji hawaruhusiwi kufanya yafuatayo:-

  1. Kuingilia shughuli za uendeshaji wa zoezi la Uboreshaji. Msimamizi wa kituo ndiye mwenye mamlaka ya mwisho juu ya nani anastahili kuandikishwa au kuboresha taarifa zake kwa mujibu wa Sheria.
  2. Kufanya kampeni za kisiasa katika kituo cha uandikishaji
  3. Kuorodhesha majina ya watu wanaojiandikisha.

Kiapo cha Kutunza Siri cha Mawakala wa Uandikishaji

Kila Wakala wa Uandikishaji kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria, ni lazima kula kiapo cha kutunza siri za taarifa za mwombaji au Mpiga Kura aliyeandikishwa. Wakala atakula kiapo mbele ya Afisa Mwandikishaji au Afisa Mwandikishaji Msaidizi. Hata hivyo, kutokuwepo kwa Wakala wa uandikishaji katika kituo cha kuandikisha Wapiga Kura hakuzuii utekelezaji wa majukumu ya Uandikishaji Wapiga Kura.

Watazamaji wa Uandikishaji

Kwa mujibu wa Kanuni ya 43(1) ya Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura za mwaka 2018 zilizoandaliwa chini ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kanuni ya 45 ya Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura za mwaka 2018 zilizoandaliwa chini ya Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Watazamaji wa ndani na kimataifa, wanaruhusiwa kutazama mchakato wa Uboreshaji utakavyofanyika katika vituo vya Uandikishaji.

Watazamaji wa Uandikishaji kabla ya kuanza kutembelea vituo vya Uandikishaji, ni lazima waombe na kupatiwa idhini ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Watazamaji. Aidha, Watazamaji 24 watakaoruhusiwa na Tume watapewa barua za kuwatambulisha kwa Maafisa Waandikishaji na Mwongozo wa watazamaji wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulioandaliwa na Tume. Maafisa Waandikishaji watatakiwa kuwapa barua za kuwatambulisha kwa Watendaji wa vituo ambavyo watavitembelea. Aidha, Watazamaji wa Uandikishaji wa Wapiga Kura hawapaswi kutoa maelekezo kwa Mwandishi Msaidizi katika kituo husika.

Kuweka Wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura

Kwa mujibu wa Vifungu vya 11A na 22 vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, na Kifungu cha 15A na 28 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Tume inatakiwa kuweka wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura ili kutoa fursa kwa wananchi:

  1. Kulikagua Daftari;
  2. Kufanya marekebisho ya majina au mahali wanapoishi;
  3. Kuingiza au kufuta majina ya Wapiga Kura;
  4. Kuweka pingamizi kwa Mpiga Kura aliyeandikishwa na hana sifa za kuwemo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Kumuwekea Pingamizi aliyeandikishwa kwenye Daftari la Awali

Kifungu cha 24 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kifungu cha 30 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 kinaruhusu Mkurugenzi wa Uchaguzi au Afisa Mwandikishaji au mtu yeyote aliyeandikishwa kuwa Mpiga Kura, kuweka pingamizi dhidi ya jina lililopo katika Daftari la Awali la Wapiga Kura. Kifungu cha 25 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kifungu cha 31 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 kinaweka utaratibu wa kuweka pingamizi. Mtu aliyewekewa pingamizi hutakiwa kupelekewa taarifa ili aweze kutoa ufafanuzi ndani ya siku saba (7).

Kifungu cha 27 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 hayo katika Mahakama ya Wilaya. Mahakama itapaswa kutoa uamuzi wa rufaa hiyo ndani ya siku 14 tangu tarehe ya kupokea rufaa hiyo, uamuzi wa Mahakama ya na Kifungu cha 33 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, vinatoa fursa iwapo aliyewekewa pingamizi hakubaliani na 25 maamuzi ya Afisa Mwandikishaji ya kuendelea kukataliwa kuwemo katika Daftari, ana haki ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi Wilaya ndiyo utakuwa uamuzi wa mwisho na mtu hatoweza kukata rufaa katika Mahakama nyingine yoyote.