Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Uwekaji Wazi Daftari la Awali

Uwekaji Wazi Daftari la Awali 

Kwa mujibu wa Vifungu vya 11A na 22 vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, na Kifungu cha 15A na 28 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Tume inatakiwa kuweka wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura ili kutoa fursa kwa wananchi:

  1. Kulikagua Daftari;
  2. Kufanya marekebisho ya majina au mahali wanapoishi;
  3. Kuingiza au kufuta majina ya Wapiga Kura;
  4. Kuweka pingamizi kwa Mpiga Kura aliyeandikishwa na hana sifa za kuwemo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Kumuwekea Pingamizi aliyeandikishwa kwenye Daftari la Awali

Kifungu cha 24 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kifungu cha 30 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 kinaruhusu Mkurugenzi wa Uchaguzi au Afisa Mwandikishaji au mtu yeyote aliyeandikishwa kuwa Mpiga Kura, kuweka pingamizi dhidi ya jina lililopo katika Daftari la Awali la Wapiga Kura.

Kifungu cha 25 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kifungu cha 31 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 kinaweka utaratibu wa kuweka pingamizi. Mtu aliyewekewa pingamizi hutakiwa kupelekewa taarifa ili aweze kutoa ufafanuzi ndani ya siku saba (7).

Kifungu cha 27 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 hayo katika Mahakama ya Wilaya. Mahakama itapaswa kutoa uamuzi wa rufaa hiyo ndani ya siku 14 tangu tarehe ya kupokea rufaa hiyo, uamuzi wa Mahakama ya na Kifungu cha 33 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, vinatoa fursa iwapo aliyewekewa pingamizi hakubaliani na 25 maamuzi ya Afisa Mwandikishaji ya kuendelea kukataliwa kuwemo katika Daftari, ana haki ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi Wilaya ndiyo utakuwa uamuzi wa mwisho na mtu hatoweza kukata rufaa katika Mahakama nyingine yoyote.