Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Historia ya Tume

KUASISIWA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

Mwaka 1991 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi aliteua Tume ya kwanza chini ya Uenyekiti wa Marehemu Jaji Mkuu Mstaafu Francis Nyalali Madhumuni ya Tume hii ilikuwa kukusanya maoni ya wananchi juu ya kuendelea na mfumo wa chama kimoja au kuwa na mfumo wa vyama vingi.

Kutokana na ushauri wa Tume ya Nyalali ,Sura ya 3 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ilirekebishwa na kufanya Tanzania kuwa Taifa linalofuata mfumo wa Vyama vingi vya Siasa.

Sheria ya Vyama vya siasa, (Na. 5ya 1992) ilirekebishwa ili kuwezesha kuandikishwa kwa vyama vya siasa. Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,(Na.1ya 1985), Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa,(Na. 4 ya 1979) na sheria zinazoendana pia zilirekebishwa ili kuondokana na matakwa ya chama kimoja na kuruhusu mchakato wa Kufanyika kwa Uchaguzi chini ya Mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Mwaka1993 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilianzishwa chini ya Ibara ya 74 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Wajumbe wa Tume waliteuliwa kwa mara ya kwanza tarehe 14 January 1993.

 

KUUNDWA KWA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni Taasisi huru ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 1993 chini ya Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977. Na Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaundwa na wajumbe wafuatao:-

i. Mwenyekiti ambaye ni lazima awe amewahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufaa ya Tanzania au mwanasheria mwenye sifa za kuwa wakili na ambaye amekuwa katika wadhifa huo si chini ya miaka 15

ii. Makamu mwenyekiti ambaye ni lazima awe amewahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufaa ya Tanzania au mwanasheria mwenye sifa za kuwa wakili na ambaye amekuwa katika wadhifa huo si chini ya miaka 15.

iii. Mjumbe aliyeteuliwa kutoka kaika chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society).

iv. Wajumbe wengine wanneni watu ambao wana uzoefu katika kuendesha na kusimamia chaguzi au sifa nyingine za ziada ambazo Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ataona zinafaa.

Kwa mujibu wa Ibara ya 74(7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na Kifungu cha 4(4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi (Na. 1 ya1985), Mkurugenzi wa Uchaguzi ndiye Katibu wa Tume ambaye pia huteuliwa na Rais.