Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Mifumo ya Uchaguzi

Mfumo wa Uchaguzi Tanzania

Tanzania inatumia Mfumo wa Uchaguzi ambao mgombea anayepata kura nyingi halali kuliko mgombea mwingine yeyote hutangazwa kuwa mshindi (First Past The Post). Hii ni kwa mujibu wa Ibara ya 41 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977, Kifungu cha 35F(8) na Kifungu cha 81 (a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kifungu cha 82 (a) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292.

Mfumo mwingine unaotumika ni wa Uwiano wa Kura (Proportional Representation) unaotumika kupata Wabunge Wanawake wa Viti Maalum ambao umetajwa kwenye Ibara ya 78 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Mfumo huu pia hutumika kuwapa Madiwani Wanawake wa Viti Maalum kama ilivyoainishwa katika Kifungu cha 35(1) (d) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura ya 287 na Kifungu cha 24(1)(c) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura ya 288.