Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Vyama 13 vya siasa vyateuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Mbarali katika uchaguzi mdogo

Imewekwa: 29 Aug, 2023
Vyama 13 vya siasa vyateuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Mbarali katika uchaguzi mdogo

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbarali Mkoani Mbeya Bw. Missana Kwangura amefanya uteuzi wa wagombea kutoka vyama 13 vya siasa kuwania kiti cha Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Mbarali unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 Septemba mwaka 2023.

Wagombea walioteliwa na vyama vyao ni Halima Abdalah Magambo (AAFP), Osward Joseph Mndeva (DP), Zavely Raurent Seleleka (UDP), Exavery Town Mwataga (CCK), Morris Thomas Nkongolo (TLP) na Modestus Dickson Kilufi (ACT Wazalendo).

Wengine ni Mary Moses Daudi (UPDP), Fatuma Rashidi Ligania (NLD), Bahati Keneth Ndingo (CCM), Bariki Oswald Mwanyalu (Demokrasia Makini), Hashim Abasi Mdemu (ADC), Mwajuma Noty Mirambo (UMD), na Husseni Hasani Lusewa kutoka Chama cha ADA- TADEA.

Baada ya uteuzi wa wagombea Msimamizi wa Uchaguzi akabandika fomu za uteuzi kwenye eneo la wazi kama inavyoekelezwa na sheria za uchaguzi ili kutoa fursa kwa vyama vya siasa, wagombea na kukagua fomu hizo.

Akizungumza baada ya uteuzi Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbarali Missana Kwangura amesema baada ya kukamilika kwa uteuzi wa wagombea, tarehe 20 Agosti mwaka 2023 kampeni za wagombea zitaanza rasmi hadi tarehe 18 Septemba mwaka 2023, hivyo amewataka wagombea na vyama vya siasa kufanya kampeni za kistaarabu.