Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Ujumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho wafanya ziara ya mafunzo Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Imewekwa: 10 Feb, 2023
Ujumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho wafanya ziara ya mafunzo Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Ujumbe wa watu wa tatu kutoka Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho (IEF Lesotho) ukuingozwa na Mjumbe wa Tume hiyo,Dkt. Karabo Mokobocho Monlakoana upo nchini kwa ziara ya mafunzo ambapo wametembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dodoma.

Katika Ziara hiyo waliyoifanya katika Makao Makuu ya Tume, ujumbe huo ulipokelewa na Mjumbe wa Tume, Asina Omar na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles na kisha kuwatembeza katika jengo hilo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Tume ya Uchaguzi Tanzania.

 

Mjumbe huyo kutoka Tume ya Lesotho, IEF Lesotho Dkt Monlakoana ameambatana na Maofisa kutoka Tume hiyo, Afisa Rasilimali watu, Thato Moete na Meneja Msaidizi wa Fedha Azael Limpho Monese.

 

Aidha ujumbe huo ulipata fursa ya kuzungumza na menejimenti ya Tume na baadae Mkurugenzi, Dkt Mahera akatoa wasilisho kuhusiana na Muundo, majukumu na Kazi za Tume.