Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Tume yatwaa Kombe Mchezo wa Kuvuta Kamba kwenye Bonanza la Ukaguzi

Imewekwa: 27 Mar, 2023
Tume yatwaa Kombe Mchezo wa Kuvuta Kamba kwenye Bonanza la Ukaguzi

TIMU ya Kamba ya Tume ya Aifa ya Uchaguzi (NEC) imefanikiwa kutwaa kombe katika Bonanza la Ukaguzi lililofanyika Jijini Dodoma na kushirikisha timu zaidi ya sita.

NEC ilitwaa ushindi huo baada ya kuwavuta kwa mivuto miwili Timu ya Ukaguzi.

Katika Mpira wa Miguu NEC hawakufurukuta mbele ya Makao Makuu Jogging baada ya kuwatupa nje kwa mikwaju ya penati ambao badae katika fainali walikutana Ugakuzi na Makao Makuu na Makao Makuu kutwaa ubingwa wa Soka.

Katika mchezo wa Mpira wa Netball timu ya Ukaguzi iliibuka kidedea baada ya kuwatndika bila huruma timu za Wizara ya Afya na Madini.

Mapema akizungumza wakati wa ufunguzi wa bonanza hilo, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere ametoa rai kwa watumishi wa umma wakiwemo wa Ofisi yake kushiri kwenye michezo kwani ni tiba isiyo na gharama.

Taasisi zilizoshiriki mbali na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Mfuko wa Bima ya Afya ya Uchaguzi(NHIF), Wakala wa Barabara(Tanroads) Ofisi ya Rais Ikulu na Wizara ya Afya.

Alisema ili kuwa na afya njema ni vyema watumishi wakashiriki mazoezi na kusisitiza kuwa mazoezi ni tiba isiyo na gharama kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza na pia kuipunguzia Serikali mzigo wa kuhudumia magonjwa hayo.

"Kazi zetu sisi Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali tunatumia muda mwingi kuandika taarifa hivyo tumekuwa tukiweka utaratibu wa kutoka nje kufanya mazoezi na ni utaratibu mzuri katika kulinda afya za watumishi."

Kichere pia alisema wanatumia bonanza hilo kujiandaa tayari na bonazan lingine litakalokutanisha na wabunge.

" Wabunge ni watu ambao tunafanya kazi nao kwa karibu, hivyo mwezi ujao tutakuwa na bonanza la kushirikiana na wabunge kwa hiyo hii ni sehemu ya mazoezi yetu."

Kichere alisema katika bonanza Hilo pia watalitumia kuchagia damu benki ya Taifa ya damu Ili kusaidia kutoka maisha ya watu wanaohitaji damu.

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya CAG, Novat Mfalamagoha kutokana na mtindo wa maisha ya mwanadamu mazoezi ni mabadala mzuri wa dawa za hospitali.

Pia alishauri wazazi kujenga tabia ya kuwashirikisha watoto kwenye mazoezi ambayo itawafanya kujenga moyo wa kupenda mazoezi.