Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Tume yashiriki warsha ya kuwajengea uwezo Tume za Uchaguzi na wadau wake kutoka Nchi za Maziwa Makuu

Imewekwa: 10 Feb, 2023
Tume yashiriki warsha ya kuwajengea uwezo Tume za Uchaguzi na wadau wake kutoka Nchi za Maziwa Makuu

Wajumbe sita (6) wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wamehudhuria Warsha ya kujengea uwezo Tume za Uchaguzi na wadau wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) inayofanyika jijini Dar es Salaam.

Wajumbe hao walioongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele, ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Rufaa Mst. Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk.

Wajumbe wengine ni Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Asina Omari, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Mwanaisha Kwariko, Mhe. Balozi Omari Ramadhani Mapuri, na Mhe. Magdalena Rwebangira.

Mkutano huo pia unahudhuriwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Charles na baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo vya Tume.