Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Tume yamteua Ndugu Aziza Sleyum Ally kuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Imewekwa: 28 Dec, 2023
Tume yamteua Ndugu Aziza Sleyum Ally kuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemteua Ndugu Aziza Sleyum Ally kuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu Ramadhani Kailima, Tume imefanya uamuzi huo leo tarehe 03 Novemba, 2023 katika kikao chake kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema uteuzi huo umefanyika kwa kuzingatia matakwa ya ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 ikisomwa pamoja na kifungu cha 86A (6) na (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

“Uteuzi huo umefanyika baada ya Tume kupokea barua yenye Kumb. Na. CEA.137/400/02A/22 ya tarehe 19 Agosti, 2023 kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoandikwa kwa mujibu wa kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.” Aliongeza Mkurugenzi wa Uchaguzi.

Kwa mujibu wa kifungu hicho, Spika aliitarifu Tume kuhusu uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kufuatia kujiuzulu aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Bahati Keneth Ndingo.