Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Tume yaamua rufaa 60 za wagombea ubunge na udiwani na kuwarejesha wagombea 34 wa udiwani kwenye uchaguzi

Imewekwa: 10 Feb, 2023
Tume yaamua rufaa 60 za wagombea ubunge na udiwani na kuwarejesha wagombea 34 wa udiwani kwenye uchaguzi

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 60 kati ya hizo rufaa ni za wagombea ubunge na 58 ni za wagombea udiwani katika kikao chake cha jana tarehe 10 Septemba 2020.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam leo tarehe 11 Septemba, 2020 na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Charles kufuatia kukamilika kwa uamuzi dhidi ya rufaa hizo.

Dkt. Charles amesema Tume katika rufaa hizo imekubali rufaa moja na kumrejesha mgombea katika orodha ya wagombea kutoka kwenye Jimbo la Iramba Magharibi na kukataa rufaa moja ya mgombea ambaye uteuzi wake ulitenguliwa kutoka kwenye Jimbo la Iramba Magharibi.

Amesema Tume imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 58 za madiwani na kukubali rufaa 34 na kuwarejesha wagombea katika orodha ya wagombea udiwani.

Amezitaja kata ambazo wagombea wake wamerejeshwa kuwa ni Kata za Kahororo (Bukoba), Ishozi (Nkenge),Chongoleani (Tanga Jiji), Kirare (Tanga Jiji), Mwamanga (Magu), Ng’haya (Magu), Riroda (Babati Vijini), Maswa Magharibi (Maswa), Kirumba (Ilemela), na kata ya Bonga (Babati Vijini).

Kata nyingine ni Kamagambo (Karagwe), Namelock (Kiteto), Masewa (Bariadi), Bweranyange (Karagwe), Kituntu (Karagwe), Kamagambo (Karagwe), Msowero (Kilosa), Lubugu (Magu), Lingeta (Meatu), Ifakara (Kilombero), Kiloli (Sikonge), Mkoma (Rorya), na kata ya Nyamhongolo (Ilemela)

Dkt. Charles amezitaja kata nyingine kuwa ni kata ya Sikonge (Sikonge), Tanganyika (Muheza), Uhenga (Wanging’ombe), Babati (Babati), Vwawa (Mbozi), Lukanga (Mkuranga), Langai (Simanjiro), Lutale (Magu), Majohe (Ilala), Namabengo (Namtumbo) na Viwanja Sitini (Kilombero).

Katika hatua nyingine, Dkt. Charles amesema pia Tume imekataa rufaa 23 za wagombea ambao hawakuteuliwa kutoka kwenye Kata za Ilemela (Ilemela), Kayenze (Mwanza Jiji), Kiarare (Tanga Jiji), Mabawa (Tanga Jiji), Ilemela (Ilemela), Kadoto (Maswa Magharibi), na kata ya Iyela (Mbeya Jiji).

Kata nyingine ambazo wagombea wake rufaa zao zimekataliwa ni kata ya Kirua Vunjo Magharibi (Vunjo), Mji Mpya (Morogoro Mjini), Pugu (Ukonga), Tembela (Mbeya Mji), Vikumburu (Kisarawe), Mecco (Ilemela), Kibara (Mwibara), Kiloleli (Sikonge), Changarawe (Mafinga Mji), Igawilo (Mbeya Mjini), Msonga (Mkuranga), Uru Kaskazini (Moshi Vijini), Kivukoni (Ilala), Maanga (Mbeya Mjini), Nsalaga (Mbeya Mjini) na Jangwani (Ilala).

“Tume pia imekataa rufaa 1 ya kupinga walioteuliwa. Rufaa hiyo ni kutoka kwenye Kata ya Arri (Babati Vijijini).Idadi hii inafanya jumla ya rufaa za wagombea Ubunge zilizofanyiwa uamuzi na Tume kufikia 113 na za wagombea Udiwani 103”, amesema Dkt. Charles.

Amesema Tume itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kila siku na kwamba wahusika wa rufaa hizo watajulishwa kwa barua juu ya uamuzi wa Tume.