Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Mwenyekiti wa Tume Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele atembelea vituo vya kupigia kura Uchaguzi Mdogo Jimbo la Mbarali

Imewekwa: 05 Oct, 2023
Mwenyekiti wa Tume Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele atembelea vituo vya kupigia kura Uchaguzi Mdogo Jimbo la Mbarali

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele leo tarehe 19 Septemba, 2023 ametembelea na kukagua zoezi la kupiga kura kwenye Jimbo la Mbarali lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.


Jaji Mwambegele baada ya kutembelea vituo amesema ameridhishwa na utendaji wa Wasimamizi wa Uchaguzi huo na kuongeza kwamba vituo vimefunguliwa kwa wakati na zoezi linaendelea vizuri kwa utulivu na amani.


Aidha, Jaji Mwambegele amezungumza na mawakala wa vyama vya siasa ambao wamemueleza kuridhishwa na mwenendo wa zoezi la kupiga kura na kwamba hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza.

Uchaguzi wa Jimbo la Mbarali unafanyika sambamba na kata sita za Tanzania Bara. Kata zenye uchaguzi ni Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mfaranyaki iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Mwaniko iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Old Moshi Magharibi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Marangu Kitowo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rombo na Mtyangimbole iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.