Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Kamati ya Bunge yatembelea Ofisi za Tume ya Tiafa ya Uchaguzi zilizoo Njedengwa jijini Dodoma

Imewekwa: 10 Feb, 2023
Kamati ya Bunge yatembelea Ofisi za Tume ya Tiafa ya Uchaguzi zilizoo Njedengwa jijini Dodoma

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Nagy Kaboyoka, imetembelea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuona Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika eneo la Njedengwa Jijini Dodoma.

Kamati hiyo ya Bunge kwa pamoja imefurahishwa sana na mradi wa Ujenzi wa Ofisi hizo za Tume zilizoko katika eneo la Njedengwa JijiniDodoma. Ambao kwa asilimia kubwa umekamilika.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles akiielezea Kamati hiyo kabla ya kuitembeza kwenye Ofisi za Tume na maandhali ya kuvutia ya nje, alisema kuwa ofisi za Tume zina Majengo matatu ambayo ni Jengo la Utawala (Main Building), Jengo la Kuhifadhia Vifaa (Warehouse) na Jengo la kutangazia matokeo (Results Center)

Mkurugenzi alifafanuwa kuwa kwa ujumla ujenzi wa majengo yote matatu unaendelea vizuri kwani majengo yako katika hatua mbalimbali ambapo hadi sasa Jengo la Utawala limekamilika kwa asilimia 99 na makabidhiano ya awali yalifanyika tarehe 22 Julai, 2020, Jengo la Kuhifadhia Vifaa asilimia 99 na Jengo la kutangazia matokeo kwa asilimia 97.

Aidha, Mkurugenzi aliielezea Kamati hiyo ya Bunge kuwa Jengo la Utawala na Jengo la Kuhifadhia Vifaa yameshaanza kutumika na inaendelea na ukamilishaji wa shughuli nyingine zinazotekelezwa na wazabuni mbalimbali.

“Tume inaishukuru serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hizi na hivyo kufanikisha Tume kuwa na majengo yake Dodoma na kwa ujumla, ujenzi wa majengo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi unaelekea kukamilika kwani umeshafikia hatua ya kumalizia shughuli ndogondogo ambazo zinatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 30, 2021 na hadi sasa mradi huu umegharimu jumla ya kiasi cha Shilingi 19,713,413,335.44 “ Alisema Mkurugenzi wa Uchaguzi

Pamoja na hayo, Mkurugenzi wa Uchaguzi aliielezea Kamati ya Bunge kuwa Tume ina uhitaji wa Ujenzi wa ofisi ndogo Jijini Dar es Salaam katika eneo lake lililopo Garden Avenue.

Mkurugenzi alifafanua kuwa ni muhimu kuwa na ofisi ndogo Dar-es-Salaam kwakuwa Tume inafanya kazi na wadau wengi ambao bado wapo Dar-es-Salaam na vifaa vingi vya uchaguzi huwa vinashushwa katika bandari ya Dar-es-Salaam.

Zaidi ya hayo, Charles alisema kuwa Tume inauhitaji wa kutatafuta eneo lililokaribu na reli ya SGR ili kujenga maghala mengine Dodoma kwa ajili ya kuiwezesha Tume kuhifadhi vifaa vyake vyote.