Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura

Imewekwa: 12 Oct, 2022

Kwa mujibu wa Kifungu cha 10 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 pamoja na kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, ili mtu aweze kuandikishwa kuwa Mpiga Kura anatakiwa kuwa sifa zifuatazo:

(i) Awe Raia wa Tanzania;

(ii) Awe ametimiza umri wa miaka 18 au zaidi; na

(iii) Awe hajapoteza sifa kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi au Sheria nyingine yoyote iliyotungwa na Bunge.1. Utaenda kituo cha kuandikisha Wapiga Kura kilichopo jirani na maeneo unayoishi.

Baada ya kutimiza sifa hizi, mtu unatakiwa kufuata utaratibu ufuatao:

1. Utaenda kituo cha kuandikisha Wapiga Kura kilichopo jirani na maeneo unayoishi.

2. Utajitambulisha kwa Mwandishi Msaidizi na Mwandishi Msaidizi atakuuliza maswali na atakujazia fomu maalum

3. Utaenda kwa BVR kit Operator kwa ajili ya kuchukuliwa alama za kielektroniki ikiwa ni pamoja na kupigwa picha

4. Utapewa kadi ya Mpiga Kura na unatakiwa uihakiki majina yako, picha na taarifa nyingine, kama kipo sahihi na baada ya kujiridhisha utaondoka kituoni.