Majukumu ya NDC ni yapi?
Kutoa fursa ya kuwaleta pamoja Maafisa Waandamizi waliochaguliwa kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na Taasisi nyingine kwa madhumuni ya kuwafunza kwa kina kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu hali ya sasa ya Usalama wa Taifa kwa ujumla na hasa Tanzania.
Kurahisisha maendeleo ya kibinafsi ya Maafisa Waandamizi waliochaguliwa wa Taasisi za Serikali na Taasisi nyingine walioteuliwa kuhudhuria mafunzo katika Chuo cha Taifa Cha Ulinzi kwa kutengeneza Chuoni mazingira mazuri ya kitaaluma kuhusiana na masuala ya Usalama wa Taifa.
Kukuza maelewano ya kina na ya kudumu kati ya Taasisi mbalimbali za Serikali na nchi rafiki zilizochaguliwa kwa kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya kazi na fursa za kuendeleza maelewano hayo kati ya maafisa wanaohudhuria mafunzo katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi.
Kuwa chombo cha Serikali cha kukuza maelewano bora, ushirikiano wa pande zote na uhusiano unaohitajika katika nyanja za usalama za kitaifa, kikanda na kimataifa na nchi za ukanda wetu.