Vigezo gani vya kujiunga na NDC?
Washiriki wa Kozi waliodahiliwa katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi kwa Kozi ya Mafunzo ya Usalama na Mikakati kwa kawaida ni wa makundi matatu yaliyochaguliwa kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wizara na Taasisi na kutoka kwa Majeshi rafiki au washirika.
Vyombo vya Ulinzi na Usalama. - Huchaguliwa na Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi kwa kawaida ni cheo cha Brigedia Jenerali au Kanali. Kwa Vyombo vya Usalama (Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto, PCCB NA TISS) ni wale waliochaguliwa na Taasisi zao ambao wamefikia cheo cha kamishna msaidizi na zaidi.
Wizara na Taasisi - Waliochaguliwa na Wizara na Taasisi ni wale maofisa ambao wana angalau shahada ya kwanza au sifa inayolingana na hiyo ya kitaaluma na ambao wamefikia ngazi ya Wakurugenzi au sawa na hayo.
Washiriki wa Kozi kutoka Majeshi Rafiki/Washirika - waliochaguliwa na mamlaka za nchi zao. Washiriki wa Kozi ya Kijeshi kutoka majeshi washirika pia ni Maafisa wa cheo cha Brigedia Jenerali au Kanali (au vinavyolingana).