Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ni taasisi ya kiserikali iliyoundwa na bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa sheria Na. 12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake ya sheria Na.6 ya mwaka 1971 na Kanuni za Baraza la Michezo la Taifa na Kanuni za usajili Na.442 za mwaka 1999 na ndio chombo pekee kilichopewa mamlaka na Bunge kusimamia Michezo nchini. Aidha Baraza la Michezo la Taifa ni Taasisi iliyopo chini ya Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo.
KAZI ZA BARAZA
Kwa mujibu wa Sheria ya Bunge Na. 12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake katika Sheria namba.6 ya mwaka 1971 kazi za Baraza ni
Kuendeleza, kustawisha na kudhibiti aina zote za Michezo ya Ridhaakwa ushirikiano na Vyama vya Michezo nchini.
Kuhimiza na kutoa fursa za ushirikiano miongoni mwa Vyama mbalimbali vya michezo vya Taifa.
Kuidhinisha Mashindano ya Kitaifa na Kimataifa katika michezo na tamasha vilivyoandaliwa na Vyama vya Taifa na Vyama vingine
Kuandaa, baada ya kushauriana na Vyama vya Ta...