Sisi ni nani

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ni taasisi ya kiserikali iliyoundwa na bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa sheria Na. 12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake ya sheria Na.6 ya mwaka 1971 na Kanuni za Baraza la Michezo la Taifa na Kanuni za usajili Na.442 za mwaka 1999 na ndio chombo pekee kilichopewa mamlaka na Bunge kusimamia Michezo nchini.  Aidha Baraza la Michezo la Taifa ni Taasisi iliyopo chini ya Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo.  KAZI ZA BARAZA Kwa mujibu wa Sheria ya Bunge Na. 12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake katika Sheria namba.6 ya mwaka 1971 kazi za Baraza ni Kuendeleza, kustawisha na kudhibiti aina zote za Michezo ya Ridhaakwa ushirikiano na Vyama vya Michezo nchini. Kuhimiza na kutoa fursa za ushirikiano miongoni mwa Vyama mbalimbali vya michezo vya Taifa. Kuidhinisha Mashindano ya Kitaifa na Kimataifa katika michezo na tamasha vilivyoandaliwa na Vyama vya Taifa na Vyama vingine Kuandaa, baada ya kushauriana na Vyama vya Taifa vinavyohusika, mashindano na matamasha ya Kitaifa na Kimataifa kwa nia ya kubadilishana uzoefu na kukuza mahusiano ya kirafiki na Mataifa mengine; Kuamsha ari kwa wananchi wote watanzania ya kupenda aina zote za michezo kwa ngazi zote. Kutoa baada ya kushauruana na vyama vya Taifa,Nishani, stashahada,vyeti,vikombe na vivutio vingine kwa ajili ya kuhimiza na kukuza shughuli za michezo Kudhamini nafasi za masomo kwa ajili ya mafunzo ya walimu wa michezo na waandaaji Kumshauri waziri kuhusu mahusiano ya nje katika uwanja wa Michezo Kushirikiana na mamlaka za serikali za mitaa ili kuwezesha kuwepo kwa fursa za michezo kwa ngazi zote na kujatahidi kujenga moyo wa uanamichezo na nidhamu kwa wanamichezo wote Kushauriana na vyama, taasisi au watu wengine kuhusiana na michezo ya ridhaa MUUNDO WA BARAZA Baraza la Michezo Taifa lina Mwenyekiti na wajumbe wa Baraza ambao huteuliwa na Waziri anayehusika na masuala ya Michezo.  Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa Baraza huteuliwa kwa kipindi cha miaka mitatu. Wakati ambapo vipindi vya kuteuliwa kwa wajumbe havina ukomo, uteuzi wa Mwenyekiti wa Baraza ni kwa vipindi viwili tu vinavyofuatana. Kwa kawaida wajumbe wa Baraza huteuliwa kwa msingi wa uwakilishi wa mikoa, asasi, asasi zinazohusiana na Michezo, idara za Serikali na asasi zisizo za Serikali.   Baraza linaongozwa na Katibu Mtendaji, ambaye ndiye Afisa mtendaji mkuu. Baraza lina idara tatu zifuatazo: i. Idara ya Maendeleo ya Michezo ii. Idara ya Utawala na Rasilimali watu.  iii. Idara ya Fedha na Mipango.  Licha ya idara hizo Tatu, kuna vitengo vitano ambavyo hufanya kazi moja kwa moja chini ya Katibu Mtendaji. Vitengo hivyo ni ; Kitengo cha Ukaguzi wa ndani Kitengo cha Manunuzi Kitengo cha Habari na Mawasiliano Kitengo cha Sheria Kitengo cha Tehama  Kitengo cha Sheria