Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MRADI WA MAJI PUGU – GONGO LA MBOTO
MRADI WA MAJI PUGU – GONGO LA MBOTO

UTANGULIZI

Mradi wa maji Pugu – Gongo la Mboto ni miongoni mwa miradi ya kimkakati iliyotekelezwa katika mwaka wa fedha 2020/21 – 2021/2022 kwa lengo la kukidhi agizo la Serikali la kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 upatikanaji wa huduma ya maji unafikia asilimia 95 kwa maeneo ya mijini.

Mradi ulisanifiwa na kutekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa kutumia fedha zilizotokana na makusanyiko ya ndani ya Mamlaka.

 

UTEKELEZAJI WA MRADI

Mradi wa maji Pugu - Gongo la Mboto umetekelezwa na DAWASA kwa lengo la kukidhi agizo la serikali la kuhakikisha ifikapo 2025 upatikanaji wa huduma ya maji kwa maeneo ya mijini unafikia asilimia 95. Mradi umetekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 6.9 ambazo ni fedha za ndani za Mamlaka.

Utekelezaji wa mradi ulihusisha kazi mbalimbali zikiwemo;

Ulazaji wa bomba kuu la inchi 16 ambalo lililazwa kwa umbali wa kilomita 13.5, sambamba na mabomba ya usambazaji maji la inchi 3 hadi 8, ambayo yamejengwa kwa lengo la kusambaza maji kwa wananchi.

Ujenzi wa bomba kuu la kusafirisha maji lenye uwezo wa kusafirisha lita 2,880,000 za maji kwa siku.

Kazi ya kufanya maunganisho mapya ya wateja 50,000 yamefanyika mara baada ya kukamilika kwa utekelezaji wa mradi, pamoja na ujenzi wa tenki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita milioni 2.

 

HALI YA MRADI KWA SASA

Mradi ulianza kutekelezwa mwaka 2019 na umekamilika kwa asilimia 100 na wananchi wanapata huduma ya majisafi.

 

MAENEO YANAYONUFAIKA NA MRADI

Mradi ulisanifiwa kwa lengo la kunufaisha wakazi 450,000 wa Kata ya Pugu, Pugu Gongo la Mboto, Chanika, Majohe, Bangulo, Ukonga, Airwing, Kinyerezi.

Mpaka sasa wateja wapatao 10,000 wamekwisha unganishwa na wananufaika na mradi huu. Kazi ya kufanya maunganisho mapya inaendelea katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mabwawa ya Samaki, Majohe kichangani, Gongo la Mboto, Kinyamwezi, Pugu station, Ulongoni B, Markaz, Mwakanga.