Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE
MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE

UTANGULIZI

Wilaya ya Kisarawe ni mojawapo ya Wilaya 8 zilizopo katika Mkoa wa Pwani. Wilaya hii ilianzishwa tarehe 1 Julai 1907 sawa na mji wa Nairobi. Mpaka sasa ni zaidi ya miaka 117 tangu ianzishwe.

 

Wilaya ya Kisarawe inapakana na Wilaya ya Mkuranga kwa upande wa Kusini – mashariki, na Wilaya ya Morogoro kwa upande wa Magharibi. Mashariki - Kaskazini kuna Jiji la Dar es Salaam, Kaskazini kuna Wilaya ya Kibaha na Kusini Wilaya ya Rufiji.

 

Wilaya hii ina eneo la ukubwa wa kilomita za mraba 3,535 na mita 1,000 juu ya usawa wa bahari. Kiutawala Wilaya ya Kisarawe imegawanyika katika tarafa nne (4) ambazo ni Sungwi, Maneromango, Mzenga na Cholesamvula. Wilaya ina jimbo moja la uchaguzi ambalo ni Kisarawe. Jimbo hili kwa sasa linaongozwa na Mbunge wa kuchaguliwa Mhe. Selemani Jafo.

 

HALI YA HUDUMA YA MAJI KABLA YA MRADI

 

Wilaya ya Kisarawe ilikuwa inahudumiwa na Mamlaka ndogo ya Majisafi (KUWSA) Kisarawe Water Supply and Sanitation Authority. Mnamo mwaka 2019, Mamlaka ndogo ya maji (KUWSA) ilivunjwa na jukumu la kutoa huduma ya majisafi katika Wilaya ya Kisarawe ilikabidhiwa DAWASA.

 

KUANZA KWA MRADI

 

Mnamo tarehe 21 Mei, 2018, DAWASA ilisaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa maji Kibamba – Kisarawe kwa lengo la kutoa huduma ya majisafi kwa wakazi wa Kibamba na Kisarawe. Ambapo Juni 27, 2018 ujenzi wa mradi ulianza rasmi na kukamilika Disemba 31, 2019.

Mradi umejengwa na mkandarasi - M/S CHICO ya China kupitia usimamizi wa Kampuni ya WAPCOS Limited ya INDIA. Mradi unazalisha lita 6,000,000 kwa siku (6,000 M3/siku). Utekelezaji wa mradi huu uligharimu shilingi Bilioni 10.64 ambazo ni fedha za Mamlaka.

Awali, kabla ya mradi huu wa DAWASA, Mamlaka ndogo ya maji iliyokuwepo ilikuwa inahudumia takribani kaya 400 katika mji wa Kisarawe, na mtandao uliokuwa na urefu wa takribani kilomita 16 na sasa DAWASA ina mtandao wenye urefu wa kilomita 148.

 

KAZI ZILIZOTEKELEZWA KATIKA MRADI;

Ujenzi wa bomba kuu la kusafirisha maji la inchi 16 kwa urefu wa km 15.65.

Ujenzi wa mabomba ya kusafirisha na kusambaza maji ya jumla ya km 34.6 kama ifuatavyo;

Ujenzi wa tenki la kuhifadhi na kusambaza maji lenye ukubwa wa mita za ujazo 6,000 (sawa na lita 6,000,000) katika eneo la Mnarani - Kisarawe. Ujenzi wa kituo cha kusukuma maji Kibamba na ofisi - Kisarawe. Ujenzi wa tenki (Sump) la kuhifadhi maji la lita 540,000 eneo la Kibamba.

 

Pia ujenzi wa tenki la kuhifadhi maji lenye ukubwa wa mita za ujazo 2,000 (sawa na lita 2,000,000) eneo la Pugu. Ufungaji wa pampu mbili (2) za kusukuma maji hadi Kisarawe. Kufunga dira (Bulk meters) kubwa nne (4) za kudhibiti matumizi ya maji.

 

Ujenzi wa matoleo (offtakes) kwa ajili ya kupeleka maji katika eneo maalum la viwanda (Visegese Industrial area) ambapo mradi huu unatarajia kufanyika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2022/23.

 

Ujenzi wa matoleo (offtakes) maalum ya kuwaunganisha Wateja maeneo mbalimbali.

Miradi 29 (line extensions) kwa ajili ya kusogeza mtandao wa maji. Mradi umekamilika kwa asilimia 100, na wananchi wa maeneo tajwa wananufaika na huduma.

 

MAENEO YANAYONUFAIKA NA MRADI

Maeneo yanayonufaika na mradi wa maji Kibamba – Kisarawe ni Wilaya ya Kisarawe katika Kata ya Kisarawe na Kata ya Kazimzumbwi, pamoja na Wilaya ya Ilala katika Kata za Pugu, Buyuni, Pugu station, Gongo la mboto, Majohe, Ukonga na Kinyerezi