ZOEZI LA KUFUATILIA MALIPO BILI ZA MAJI
02 Feb, 2024
Zoezi la ufuatiliaji wa madeni na malipo ya bili za huduma ya maji kwa wateja likiendelea katika mkoa wa kihuduma DAWASA Mkuranga.
Zoezi hili limeambatana na utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya maji, utunzaji wa maji, ulinzi wa miundombinu ya maji pamoja na kusitisha huduma kwa wateja wenye malimbikizo ya madeni ya bili.
Mamlaka inasisitiza wananchi kulipa bili zao kwa wakati ili kuepukana na usumbufu wa kusitishiwa huduma kutokana na bili kutolipa kwa wakati.