WEWE NI MKAZI WA MUHEZA HADI VISIGA WILAYANI KIBAHA NA ULIOMBA HUDUMA YA MAJI DAWASA?
09 Oct, 2023
Habari njema kwa wakazi wote wa maeneo ya
Muheza, Mailimoja, Visiga, Simbani, Kongowe, Mwambisi, Zegereni na
Galagaza kuwa ofisi ya DAWASA KIBAHA inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi.
Pamoja na zoezi hilo, elimu mbalimbali zinatolewa ikiwa ni pamoja na elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasiliano na malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.
Zaidi ya wateja 150 wanatarajia kuanza kunufaika na huduma ya majisafi.
Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0734 460 022 (DAWASA Kibaha).