WATUMISHI MABWEPANDE WAKUMBUSHWA MISINGI YA HUDUMA BORA
Katika kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoadhimishwa kila tarehe 2-6 Oktoba ya kila mwaka, Mkoa wa kihuduma DAWASA Mabwepande imetoa mafunzo kwa watumishi wake juu ya umuhimu wa kutambua haki na wajibu wa Mamlaka kwa wateja pamoja na usimamizia wa miongozo ya utumishi wa umma ili kukidhi viwango na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mafunzo haya yameongozwa na Afisa huduma kwa wateja, DAWASA-Mabwepande Bi Blandina Shelutete ambaye amesisitiza uwajibikaji katika kusimamia misingi ya utoaji huduma za Maji bila upendeleo.
“Tutumie wiki hii ya huduma kwa Wateja kusimamia uimarishaji wa huduma kwa wateja na utoaji huduma kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ili kuepuka upendeleo na malalamiko ya wananchi tunaowahudumia” alisisitiza Bi Blandina
Wiki ya huduma kwa wateja mwaka 2023 imebeba kauli mbiu inayosema "Huduma kwa Ushirikiano,".