Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
WAKAZI WA KINYAMWEZI NA MWAKANGA HUDUMA YAWAFIKIA 
06 Sep, 2023
WAKAZI WA KINYAMWEZI NA MWAKANGA HUDUMA YAWAFIKIA 

Habari njema kwa wakazi wa maeneo ya Kinyamwezi, Majohe, Pugu Stesheni, Mwakanga na Gongo la Mboto, Jimbo la Ukonga, Wilaya ya Ilala mnataarifiwa kufika ofisi za DAWASA Ukonga ili kupata vifaa vya maunganisho mapya ya majisafi. 

Leo zoezi la utoaji wa vifaa limefanyika kwa wananchi 50 wa maeneo tajwa, sambamba na utoaji wa elimu ya utunzaji wa miundombinu ya majisafi na kutoa taarifa kwa Mamlaka palipo na uvujaji wa maji. 

Kwa msaada na taarifa zaidi kuhusu huduma wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) na 0739-038493 DAWASA Ukonga.