Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
WAKAZI MSANGANI HADI VISIGA WAITWA MAUNGANISHO MAPYA YA MAJI 
29 Sep, 2023
WAKAZI MSANGANI HADI VISIGA WAITWA MAUNGANISHO MAPYA YA MAJI 

Habari njema kwa wakazi wa maeneo ya Visiga, Kongowe, Mwambisi, Soga, Vikuge, Miembesaba, Kwamfipa, Galagaza, Zegereni, Mailimoja, Muheza na Msangani kuwa ofisi ya DAWASA KIBAHA inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi. 

Pamoja na zoezi hilo, elimu ya utunzaji wa miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasiliano,  malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA. 

Jumla ya wateja 95 wa maeneo hayo wanatarajiwa kunufaika na huduma ya majisafi.

Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0734 460 022 (DAWASA Kibaha).