WAKAZI MBEZI MSUMI - MAVURUNZA KUPATA MAUNGANISHO MAPYA MAJI
Habari njema kwa wakazi wa maeneo ya Mbezi msumi, Mshikamano, mikoroshini, Kwa paulo, Msakuzi-machimbo, Kwa mpogoro, Msakuzi- upendo, Baruti, Bonyokwa, Mavurunza na Kimara mwisho Wilaya ya Ubungo kuwa DAWASA UBUNGO imeendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya majisafi kwa lengo la kufikisha huduma kwa wakazi wote.
Kupitia zoezi hilo, elimu mbalimbali zimetolewa kwa wateja wapya ikiwemo elimu ya utunzaji wa miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasiliano, njia za malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.
Zaidi ya wateja 160 wa maeneo tajwa wanatarajiwa kuanza kunufaika na huduma ya majisafi.
Kwa msaada na taarifa zaidi kuhusu huduma wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) na 0735 451 865 (DAWASA Ubungo).