WAKAZI 300 NJIA PANDA, TEGETA A WAONJA MAJI MRADI MAKONGO BAGAMOYO
15 Sep, 2023
Kazi ya kulaza bomba za inchi 3 kwa umbali wa mita 800 ikitekelezwa kwa lengo la kusogeza huduma ya Majisafi kwa wakazi wa njia Panda, Tegeta “A” ambao ni sehemu ya wanufaika wa mradi wa usambazaji maji Makongo hadi Bagamoyo.
Maboresho haya yanayotekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA - Makongo yanalenga kufikisha huduma kwa wakazi takribani 300 wa eneo tajwa.
Mradi wa usambazaji maji Makongo hadi Bagamoyo ni miongoni mwa mradi wa kimkakati uliotekelezwa na Mamlaka kwa lengo la kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji hususani katika maeneo ya Goba na Tegeta A.