WAILES HADI VITUKA WASOGEZEWA HUDUMA YA MAJI
18 Apr, 2024
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeendesha zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya majisafi kwa wateja wapya wa maeneo ya Vituka, Amani, Nyambwela, Yombo, Minazi mirefu, Keko machungwa, Machimbo, Sigara na wailes
Jumla ya wateja 31 wa maeneo hayo sasa wananufaika na huduma ya majisafi baada ya kukamilika kwa zoezi hili.
Sambamba na kazi hii, elimu mbalimbali zimetolewa ikiwa ni pamoja na elimu ya utunzaji wa miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasiliano, malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.