WADAIWA SUGU WAFIKISHWA MAHAKAMANI - MLANDIZI
16 Feb, 2024
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa kihuduma DAWASA Mlandizi imewafikisha mahakamani wateja takribani 50 wenye madeni sugu wanaohudumiwa katika mji huo.
Wateja wameitikia wito na kufika mahakamani ambapo wamekubali uhalali wa madeni, miongoni mwao kuahidi kulipa madeni na wengine kuingia mkataba na Mamlaka ya kulipa ndani ya muda uliowekwa kisheria.
Aidha, wateja wamepewa muda wa siku kadhaa na Mahakama ya Mlandizi kufanya malipo na kufika kortini wakiwa na risiti zao halali za malipo ndipo kesi zao zitaruhusiwa kusikilizwa.