Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
UZALISHAJI MAJI RUVU CHINI WAREJEA KATIKA KAWAIDA YAKE
28 Feb, 2024
UZALISHAJI MAJI RUVU CHINI WAREJEA KATIKA KAWAIDA YAKE

Kazi ya Marekebisho ya Pampu ya kusukuma maji katika mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini imekamilika. Marekebisho haya yaliyopelekea upungufu wa uzalishaji maji kutoka lita milioni 270 hadi lita milioni 220 kwa siku.

Matengenezo yamekamilika leo, February 26, 2024 na kurudisha hali ya uzalishaji katika kawaida yake ya ujazo wa lita milioni 270 kwa siku.

Maeneo yafuatayo yataanza kupata huduma ya maji kwa msukumo mzuri
Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo, Kikuu, Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala na Katikati ya Jiji.