USOMAJI MITA ZA MAJI SHIRIKISHI
19 Mar, 2024
Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inaendelea na zoezi la usomaji wa mita za Maji kwa kushirikiana na wateja ambapo watumishi wa Mkoa wa kihuduma DAWASA Mapinga na Chalinze wametekeleza kwa kutembelea wateja wao.
Mamlaka inatoa rai kwa wateja wote wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kutoa ushirikiano kwa watumishi watakapo kuwa wanapita katika maeneo yao wakati zoezi hilo likiendelea.
Kwa msaada wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) na 0735-202121 WhatsApp tu.