USOMAJI MITA SHIRIKISHI UNAENDELEA KIBAHA
22 Apr, 2024
Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inaendelea na zoezi la usomaji wa mita za Maji kwa kushirikiana na wateja ambapo watumishi wa Mkoa wa kihuduma DAWASA Kibaha wanatekeleza zoezi hilo kwa vitendo.
DAWASA inatoa rai kwa wateja wote wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kutoa ushirikiano kwa watumishi pindi wanapopita katika makazi yenu wakati zoezi hilo likiendelea.
Kwa msaada wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064(Bure) na 0735-202121 WhatsApp tu.