Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
USIKU NA MCHANA KUIMARISHA HUDUMA YA MAJI TABATA
06 Oct, 2023
USIKU NA MCHANA KUIMARISHA HUDUMA YA MAJI TABATA

Katika kuhakikisha Mamlaka inafikisha huduma bora kwa mwananchi, DAWASA inaendelea na kazi ya ujenzi wa kituo cha kusukuma maji (booster pump) kwenye bomba la inch 48 na kutoa toleo kwenye bomba la inch 8 kazi inayofanyika eneo la Kifuru Soweto, Kata ya Kwembe Wilaya ya Ubungo.

Lengo la kazi hii ni kuongeza msukumo wa maji uweze kufika katika maeneo mengi.

Kukamilika kwa kazi hii kutaimarisha huduma wakazi wa maeneo ya King'azi B, Kinyerezi, Kifuru, Msigwa, Kibaga B, Kibaga Juu na Kinyerezi Kanga Juu