USAFISHAJI DIRA ZA MAJI
24 Apr, 2024
Zoezi la kusafisha dira za maji zenye changamoto mbalimbali kama vile ukungu, na kujaa mchanga, linaendelea katika eneo la Mkoa wa kihuduma DAWASA - Mabwepande katika Wilaya ya Kinondoni.
Lengo la ukaguzi wa dira ni kuongeza ufanisi, kuzuia upotevu wa maji pamoja na kurahisisha usomaji wa dira utakaoleta matokeo chanya.
Zoezi hili linaenda sambamba na ukusanyaji wa ankara za Maji za mwezi.