UPOTEVU WA MAJI UNADHIBITIWA MIVUMONI
19 Jan, 2024
UPOTEVU WA MAJI UNADHIBITIWA
Fundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA), Ndugu George Suitbet akizuia upotevu wa maji eneo la Mtaa wa Kilimahewa kata ya Mivumoni, wilayani Kinondoni.
Kukamilika kwa kazi hii kutaboresha upatikanaji wa huduma kwa wakazi wa mtaa huo.
Mamlaka inatoa wito kwa Wananchi kuendelea kutoa taarifa za mara kwa mara juu ya upotevu wa maji ili yathibitiwe na yaweze kuwafikia wengi.