Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
UJENZI WA KITUO CHA KUSUKUMA MAJI BONYOKWA, KAZI IMEKAMILIKA - UBUNGO
18 Mar, 2024
UJENZI WA KITUO CHA KUSUKUMA MAJI BONYOKWA, KAZI IMEKAMILIKA - UBUNGO

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imekamilisha ujenzi wa kituo cha kusukuma maji (booster pump) katika eneo la Mavurunza kata ya Bonyokwa wilayani Ubungo utakaosaidia kuongeza upatikanaji wa maji kwa takribani wateja 12,000 katika maeneo ya Bonyokwa kwa kichwa, Bonyokwa stand, Bonyokwa mnara wa Voda, Bonyokwa Kisiwani juu na chini, Chuo cha Masanja, Canada, Macedonia, viwanja vya bank, Shedafa, JKT B, Msikiti wa kijani, Mwisho wa lami na viwanja vya JKT.

Ujenzi wa kituo hicho chenye ujazo wa lita laki na nusu, ujazaji wa maji, ufungaji wa transfoma pamoja na ujenzi wa chumba cha kuendesha pump umekamilika na unatarajia kuunganishwa na nishati ya umeme hivi karibuni.