UJENZI MAJI HOUSE WAFIKIA ASILIMIA 95
06 Oct, 2023
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Ndugu Kiula Kingu amekukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la "Maji House" lililo katika hatua za mwisho za utekelezaji.
Mradi huu unatekelezwa na mkandarasi kampuni ya Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) ambapo kwa sasa imefikia zaidi ya asilimia 95 ya utekelezaji.