UHAMASISHAJI WA ULIPAJI ANKARA ZA MAJI MKURANGA
19 Jan, 2024
UHAMASISHAJI WA ULIPAJI ANKARA ZA MAJI MKURANGA
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kupitia mkoa wa kihuduma Mkuranga inaendelea na zoezi la kuhamasisha ulipaji wa ankara za maji kwa wateja waliositishiwa huduma ya maji kutokana na malimbikizo ya muda mrefu katika eneo la Mkuranga Mjini.
Zoezi hilo limeenda sambamba na kutoa wito kwa wateja waliositishiwa huduma kuingia makubaliano na Mamlaka ha kulipa bill zao kwa muda maalum ili waendelee kupata huduma ya majisafi na salama na kuepuka madhara ya kutumia maji yasiyo salama kwa afya zao.
Zoezi hili litaendelea katika kata zote sita, ambazo ni Mkuranga mjini, Kiparang'anda, Mipeko, Vikindu, Vianzi na Mwandege zinazohudumiwa na Mamlaka.