UFUATILIAJI MAKUSANYO YA ANKARA ZA MAJI
28 Feb, 2024
Zoezi la ufuatiliaji wa madeni na malipo ya bili za huduma ya maji kwa wateja likiendelea katika mkoa wa kihuduma DAWASA Bagamoyo.
Zoezi hili limeambatana na utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya maji, utunzaji wa vyanzo vya maji, ulinzi wa miundombinu ya maji, umuhimu wa kulipa bili za maji kwa wakati pamoja na kusitisha huduma kwa wateja wenye malimbikizo ya madeni ya bili.
Mamlaka inasisitiza wananchi kulipa bili zao kwa wakati ili kuepukana na usumbufu wa kusitishiwa huduma kutokana na bili kutolipa kwa wakati.