UDHIBITI UPOTEVU WA MAJI KIZUIANI
22 Apr, 2024
Kazi ya kudhibiti upotevu wa maji katika bomba la inchi 4 eneo la Kizuiani ikiendelea kutekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).
Kukamilika kwa maboresho hayo kutaimarisha msukumo wa maji kwa wakazi wa maeneo ya Kizuiani, Kipati, Moringe na Sabasaba.
DAWASA inaendelea kuwasihi wananchi kutoa taarifa za mara kwa mara endapo watabaini uvujaji katika maeneo yao kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (bure) na mitandao ya kijamii ya mamlaka.