UDHIBITI UPOTEVU WA MAJI - BAGAMOYO
08 Mar, 2024
Kazi ya matengenezo kwenye bomba ya inch "6" ikiendelea kwa lengo la kudhibiti upotevu wa maji eneo la Kichemchem, Sabibo kata ya Bagamoyo mjini.
Kukamilika kwa matengenezo hayo kutaimarisha usambazaji wa huduma ya maji kwa wakazi takribani 1020 wa maeneo ya Mtambani, Nianjema, Kimalang'ombe, Kidogo Chekundu, Sanzale, Stendi ya Kongoe na Kigongoni pamoja na kuboresha huduma katika maeneo hayo.