UDHIBITI UPOTEVU WA MAJI
06 Sep, 2023
Kazi ya matengenezo ya valvu ya bomba la inchi 6 kutoka kwenye bomba la inchi 12 lililopo Makongo juu kwa lengo la kudhibiti upotevu wa maji, kwenye eneo la Kwa Sanya, kata ya Mbezi Juu Wilaya ya Kinondoni.
Kazi hii inatekelezwa na Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Kawe ili kuimarisha upatikanaji wa huduma.
Kukamilika kwa matengenezo hayo kutaboresha huduma ya majisafi kwa wakazi takribani 1420 wa maeneo tajwa, mtaa wa maendeleo, kwa pembe Baraza la mitihani, Kayuni, Mkomna, Libra, Mji mpya na Mnara wa Vodacom.
Kwa mwaka huu wa fedha 2023/24, Mamlaka imewekeza nguvu kubwa katika kudhibiti upotevu wa majisafi ili kuimarisha huduma kwa wananchi wote.