UBORESHAJI WA HUDUMA YA MAJISAFI KINZUDI
24 Apr, 2024
Kazi ya maboresho ya miundombinu ya majisafi kwa kutekeleza kazi ya kulaza bomba za inchi 12 kwa umbali wa Kilomita mbili ikiendelea kupitia Mkoa wa kihuduma DAWASA -Mivumoni.
Utekelezaji wa kazi hii imefikia asilimia 87 na kukamilika kutaboresha huduma kwa kuongeza msukumo wa maji kwa wakazi wa maeneo ya Usukumani, Goba Maghorofani, Tatedo, pamoja na Kinzudi.